Kocha wa Mbao FC Atamba Kulipa Kisasi Kwa Yanga - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kocha wa Mbao FC Atamba Kulipa Kisasi Kwa Yanga

OKTOBA 30, mwaka jana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Mbao FC ilifungwa mabao 3-0 na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, sasa Mbao FC imesema inataka kulipa kisasi.

Katika mchezo huo, mabao ya Yanga yalifungwana Vincent Bossou dakika ya 49, kipa wa Mbao,
Emmanuel Shija alijifunga dakika ya 55 na Amissi Tambwe alifunga bao la tatu dakika ya 75, mchezo ukaishia hapo.

Kesho Jumapili Mbao itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa na Mbao imepanga kulipa kisasi kwa gharama yoyote ile.

Kocha wa Mbao, Ettiene Ndayiragije, raia wa Burundi, aliyewahi kuwafundisha Laudit Mavugo wa Simba na Tambwe wa Yanga wakati anaifundisha Vital’O ya nchini kwao, amesema: “Lazima tuifunge Yanga.

” Ndayiragije alisema atahakikisha wanaifunga Yanga katika mchezo huo ili timu yake iweze kutinga fainali ya Kombe la FA ili inufaike na mambo mawili ambayo ni kulipa kisasi, pia kucheza Kombe la Shirikisho Afrika wakitwaa ubingwa.

Ndayiragije alisema: “Naiheshimu Yanga kutokana na uwezo wake uwanjani, lakini mimi nimeiandaa timu yangu kulipa kisasi pia tufike fainali, nashukuru wachezaji wagonjwa wengi wamepona.”

Miongoni mwa wachezaji wagonjwa waliopona ni Asante Kwasi aliyeumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao walifungwa kwa mabao 3-2.

“Niwaombe wadau wetu wajitokeze kwa wingi kutusapoti nadhani wanatufahamu jinsi ambavyo hatutaki mchezo hasa kwenye michezo hii mikubwa, waje hatutawaangusha,” alisema Ndayiragije.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.