Kipigo chasababisha Borussia Dortmund kuitupia lawama UEFA. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kipigo chasababisha Borussia Dortmund kuitupia lawama UEFA.

\
Wakiwa nyumbani kwao Dortmund walikubali kipigo cha mabao 3 kwa 2 toka kwa wakali wa Ufaransa Monaco. Mchezo ambao ulipaswa kuchezwa siku ya Jumanne lakini kutokana na mlipuko wa bomu karibu na basi la Dortmund ukapigwa Jumatano.

Kocha wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel amesema kipigo toka kwa Monaco lawama ziwaendee UEFA. Tuchel anadai baada ya tukio la mlipuko, chama hicho cha soka cha Ulaya kililichukulia tukio hilo kikawaida sana na wala hawakuipa Dortmund umuhimu mkubwa.

Tuchel anasema kikosi chake hakikuwa tayari na mchezo kupigwa siku ya Jumatano kwani wachezaji hawakuwa sawa kiakili, lakini UEFA badala ya kukaa chini wao kama wahanga wa tukio na kuwauliza nini cha kufanya?FIFA walifanya maamuzi wenyewe bila kuwashirikisha.

“Hawakutuuliza nini cha kufanya, walikaa wenyewe wakafanya maamuzi kisha baadae wakatutumia ujumbe kwamba mechi itachezwa siku ya Jumtano, ilitunyong’onyeza lakini hatukuwa na jinsi lakini kitendo cha mechi kupangwa bila kutushirikisha haikuwa sawa” alisema Tuchel.

Kauli ya Tuchel inapingana na kauli ya awali ya UEFA ambao walisema kabla ya mchezo huo kwamba, baada ya tukio la mlipuko kutokea waliwaita Monaco na Dortmund na kukaa nao chini ambapo walikubaliana kwa pamoja kwamba mchezo urudiwe siku inayofuata.

Kipigo cha nyumbani kutoka kwa Monaco kimeiweka katika hatari ya kutolewa katika Champions League, lakini Tuchel anaamini hiyo ilikuwa kama kipindi cha kwanza na cha pili ni nchini Ufaransa watapambana ili kusonga mbele.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.