Kilichokwamisha ngoma ya Darassa, hiki hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kilichokwamisha ngoma ya Darassa, hiki hapa

Darassa

Mtayarishaji wa video nchini  Hanscana ambaye pia ni mdau wa lebo ya CMG ya rapa Darassa amefunguka kuwa msanii huyo ameshindwa kuachia wimbo mpya mwezi huu kutokana na kuwa na show nyingi za kimataifa kumbana.

Hascana ameongea hayo hivi karibuni na kudai kuwa rapa huyo  tayari amesha-'shoot' video kadhaa za nyimbo zake ambazo hajazitoa bado.

“Kusema kweli Darassa alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini show za Rwanda na Burundi zimembana sana, amekuwa na tour ndefu sana katika nchi hizo na pia baadaye ataenda Kenya. Tour zikiisha tu ataachia kazi mpya kwa sababu ndani tuna kazi nyingi kali, ni kitendo cha kuzitoa tu,” alisema Hanscana

Rapa huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya kitendo ambacho kimewafanya mashabiki wa muziki kumsubiria kwa hamu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.