Kamanda Sirro kumaliza 'utata' wa alipo Roma - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kamanda Sirro kumaliza 'utata' wa alipo Roma

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Jumamosi hii atakutana na wasanii kuwaeleza taarifa ya jeshi hilo kuhusiana na kupotea kwa rapper Roma Mkatoliki na wengine waliotekwa na watu wasiojulikana usiku wa Jumatano katika studio za Tongwe Records.

Katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, Katibu Mkuu wa chama cha wasanii wa kizazi kipya, TUMA, Samweli Andrew Mbwana maarufu kama Brighton amesema amefanikiwa kuongea na Kamanda Sirro Ijumaa hii.

“Yeye [Sirro] ametusisitiza kwamba tuendelee kuwa na uvumilivu hili suala wao wanalishughulikia, na bahati nzuri wao kama polisi wameshapata taarifa zetu, wameshafungua jalada,” amesema Brighton.

“Simon Sirro ametuhakikishia hilo, yuko na chombo, ameunda chombo maalum katika kuhakikisha kwamba hawa ndugu zetu wanapatikana salama. Na vile vile ametuahidi kesho saa tano na nusu wote kwa umoja wetu, wasanii pamoja na ndugu zetu waandishi wa habari tufike ofisini kwake pale ataweza kutupa taarifa ya hali inavyokwenda na wapi amefikia kama amewapata ama kuna taarifa yoyote kuhusu wao ambao wamepotea,” ameongeza.

Brighton ameiomba jamii kuwaunga mkono wasanii hao kuhakikisha Roma na wenzake wanapatikana wakiwa salama. Wengine waliopotea ni rapper Moni Centrozone, producer wa Tongwe Bin Laden wengine watatu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.