Jay Moe: Nilipata Aibu Kwa Bill Nas - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jay Moe: Nilipata Aibu Kwa Bill Nas

RAPA aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Mvua na Jua’, Juma Mchopanga (Jay Moe), amesema licha ya kutamani kufanyakazi na rapa wa wimbo wa ‘Sitaki Mazoea’, William Lyimo (Bill Nas), hatasahau alivyomdharau kabla ya kusikiliza na kuona video zake.

Jay Moe alisema kabla ya kumwona, kusikiliza na kutazama video zake hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alipotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake alidharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini.
“Unajua kuna siku meneja wake, Bill Nas ‘Mchafu’, alinitumia wimbo akiniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo, nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wapo kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania.
“Hapo nikajifunza kitu kuwa hutakiwi kumdharau mtu, maana dogo ana uwezo mkubwa wa kurap na anajua nini anafanya hadi nimemwahidi kufanya naye kazi,” alisema Jay Moe.
Rapa huyo anayetamba na wimbo wa ‘Nisaidie Kushare’, aliongeza kwamba licha ya kutamani kufanya naye kazi pia anatamani kumtungia mashairi Bill Nas kama atakuwa tayari.
Mtanzania

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.