Huwezi amini sio La Liga wala Epl inayoongoza kwa msisimko Ulaya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huwezi amini sio La Liga wala Epl inayoongoza kwa msisimko Ulaya.

Watu wengi wanaiongelea ligi ya Uingereza na Hispania kama ligi bora duniani kwa sasa, wengi wanasema ligi hizo mbili ndio zinazovutia kuziangalia humu duniani

Lakini huwezi kuamini utafiti uliofanywa na CIS Football Obsevartory umeonesha kwamba ligi kuu ya Uswisi ndio ligi inayovutia kutokana na msisimko wake kuiangalia sana barani Ulaya

Utafiti huu umefanywa hasa kwa kuzingatia magoli katika ligi, kwa kuwa magoli ndio hufanya soka livutie baasi ligi ya nchini Uswisi inavutia sana kuitazama kwa sasa kwani ina wastani wa 3.33 ya magoli kwa mechi.

Ligi ya Hispania almaarufu kama La Liga iko nafasi ya 3 ikiwa na wastani wa magoli 2.90 kwa mechi, La Liga iko nyuma ya ligi ya Sweden ambayo ina wastani wa 3.01 kwa kila mechi.

Ligi inayoitwa tamu ya Uingereza iko nafasi ya 6 katika utafiti huu wa ligi zinazovutia huku Epl ikiwa na wastani wa 2.84 ikifuatiwa na ligi ya Serie A Italia ambayo yenyewe ina wastani wa 2.80.

Ligi ya Ubelgiji anayochezea Mbwana Samatta iko nafasi ya 10 ikiwa na wastani wa 2.74, ikiwa juu ya ligi kubwa kama Bundesliga iliyo nafasi ya 12 ikiwa na wastani wa 2.71.Ifuatayo ni 10 bora ya ligi zenye msisimko kuangalia kutokana na utafiti wa CIES.

1.Swiss Super League.

2.Swiddish Allsvenskan.

3.La Liga.

4.Norwegian.

5.Cypriot Championship.

6.EPL.

7.Serie A.

8.Polish Ekstraklasa.

9.Dutch Eredvise.

10.Belgium Pro League.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.