Hatimaye Siri ya Diamond Platnumz na Future Yafichuka. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hatimaye Siri ya Diamond Platnumz na Future Yafichuka.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz baada ya ujumbe na tetesi za muda sasa ameweka mambo sawa kuwa ni kipi kitafanyika kati yake na rapa kutoka Marekani ‘Future.’

Kupitia mitandao ya kijamii Diamond ametangaza kuwa tarehe(22 ya mwezi Julai) iliyotajwa kipindi cha nyuma kuhusu ujio wake na rapa Future amethibitisha kuwa watapaeform katika tamasha la Castle Lite litakayofanyika jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders Club.

Vile vile show hiyo inayotazamiwa kuwa kubwa ambapo pia ilitangazwa na kampuni ya vinywaji ya Castle Lite Tanzania kupitia ukurasa wa Twitter na inayoonekana kuwa wapo katika ufanikishaji wa kolabo la jukwaa la Diamond Platnumz na rapa Future.

Vifuatavyo ni uthibitisho vya ujio wa Diamond Platnumz na rapa Future.

DAR ES SALAAM!!!! DAR ES SALAAM!!!! YOU KNOW HOW HOW MUCH I MISS YOU RIGHT?????? SEE ON THE 22ND JULLY 2017 AT LEADERS CLUB KINONDONI!!! 💥🕵🔫
Posted by Diamond Platnumz on Thursday, April 20, 2017

Hata hivyo ni wengi wameshuhudia pindi tu Diamond anapopata nafasi ya kukutana na wafanya biashara wenzake lazima atupe karata ya kufanya biashara zaidi kwa kila namna hivyo haitakuwa ajabu sana kwake kufanya mengi zaidi na Future katika siku za usoni baada ya onyesho hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.