Harmorapa Afunguka Kuhusu Utajiri Alionao na Suala la Yeye Kumiliki Bastola. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmorapa Afunguka Kuhusu Utajiri Alionao na Suala la Yeye Kumiliki Bastola.

Harmorapa amefunguka kuhusu kumiliki bastola yake binafsi.Rapper huyo machachari ambaye kila kukicha huteka vichwa vya habari kutokana na vituko vyake, amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One,japo ana mali nyingi kwa sasa lakini hafikirii kuwa na bastola kwakuwa ana ulinzi wa kutosha.

“Sasa hivi nina pesa nyingi, nina gari nini. Lakini sijawaza au kufikiri siku nije kumiliki bastola kwa sababu eti nina pesa sijawaza kwa muda huu ila sijajua huko mbeleni iatkuwaje,” amesema Harmo.

“Nikisema kwaajili ya kujilinda unajua sasa hivi mimi nina bodyguard wangu ameshiba na ameenda hewani. Hata ninapokaa kwenyewe nina ulinzi mpaka umfikie Harmorapa kuna kazi kubwa sana na unaweza usionane naye,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.