Diamond, Future jukwaa moja Julai - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond, Future jukwaa moja Julai

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' na Rapa Future kutoka Marekani wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha maalumu litakalofanyika Julai 22 jijini Dar es Salaam.

Mbali na wasanii hao pia wasanii wengine wa muziki wa Hip Hop na RNB wa hapa nchini watakaotangaza hapo baadaye watatoa burudani kwenye tamasha hilo.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Afrika Mashariki, Thomas Kamphuis, alisema mbali na kutoa burudani kwa wateja wa kampuni hiyo, pia watalenga kutangaza bia mpya ya Castle lite Unlock.

“Lengo ni kuwakutanisha wateja wetu kwa pamoja katika tamasha hilo lakini pia kuitangaza bia yetu ambayo inaendelea kuwa katika ubora unaokubalika,” alisema.

Naye Meneja Masoko wa TBL, Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe, alisema kabla ya tamasha hilo, wateja wa bia hiyo watakuwa wakijishindia zawadi mbalimbali.

Kavishe alisema ili mteja kupata zawadi hizo katika kipindi hicho, akinywa kinywaji hicho atakuta namba chini ya kizibo ambayo itamuwezesha kujishindia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.