Chirwa aanza mazoezi na Yanga baada ya kumaliza mgomo wake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chirwa aanza mazoezi na Yanga baada ya kumaliza mgomo wake

Hatimaye mshambuliaji Obrey Chirwa ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga.

Yanga imeanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road na Chirwa aliyegoma safari ya Algeria akiungana na wenzake.

Chirwa raia wa Zambia aligoma kwenda ALgeria alitaka kulipwa mshahara wake ambao haukuwa umelipwa.

Aligoma kutoa pasi yake ya kusafiria kwa viongozi wa Yanga ili kuanza maandalizi ya safari.

Lakini leo, Chirwa akiwa pamoja na Vicent Bossou wameanza mazoezi na kikosi kizima cha Yanga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.