Brazil Vinara wa Soka Duniani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Brazil Vinara wa Soka Duniani

Nyota wa Brazil kutoka kushoto Philippe Coutinho, Neymer Jr na Gabriel Jesus

Timu ya taifa ya Brazil wamekua vinara wa soka kwa mwezi wa Machi kwa viwango vinatolewa na Fifa.

Wacheza samba hao wamerejea kileleni kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 6 na imekua timu yenye mafanikio kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa kombe la dunia la 2018.

Argentina wako nafasi ya pili, Ujermani wako nafasi ya tatu, Chile wako nafasi ya nne huku Colombia wakiwa katika nafasi ya tano. 6. Ufaransa 7. Ubelgiji i 8. Ureno 9.Uswisi 10.Hispania.

Misri wako juu kwa bara la afrika wakiwa nafasi ya 19 wakifuatiwa na Senegal 30 , mabingwa wa Afrika Cameroon wako nafasi ya 33.

Kwa upande wa Afrika Mashariki Uganda the Cranes iko nafasi ya 72 ikiwa imepanda nafasi 3, Kenya nafasi iko 78,Rwanda inakamata nafasi ya 117 ikiwa imeshuka kwa nafasi 17.
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania

Tanzania imepanda kwa nafasi 22 toka 157 mpaka nafasi ya 135, Burundi imeporomoka kwa nafasi 3 kutoka nafasi ya 138 mpaka 141.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.