BillNass: Nyimbo Zangu Zitumike Kama Funzo Mitaani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

BillNass: Nyimbo Zangu Zitumike Kama Funzo Mitaani

Rapper anaefanya vizuri kwasasa tatika tasnia ya muziki mkali Billnass a.k.a Billnenga ameamua kutoa matumizi sahihi na nyimbo zake na ameomba zitumike kama ujumbe wa nyimbo unavyosema.

Mkali huyo ambae ameachia 'Aje mwenyewe' wiki hii ameomba nyimbozake zitumike kama funzo mitaani kutokana na ngoma zake zote ni miongoni mwa mambo yanayotokea katika maisha yetu ya kila siku.

Ligi ndogo: Hii ilisimama kama ngoma yenye ujumbe ambao unaomba mtu asipende kufanya ushindani kwa vitu vidogovidogo ambavyo mwisho wa siku vitakuwa havina maana katikan maisha.

SitakiMazowea: Hivi unajua unapozoweana sana na watu ndo uhasama unapoanzia hapo nahata kushidwa kupeana kipaombele na baadae kuaribiana Cv.

AjeMwenyewe: Kwa maisha yetu wengi wamezowea kutumiana mtu ili kumfikishia ujumbe, Sasa kwenye hili Billnass hakubaliani nalo kama unajambo ni bora umfate mtu direct na sio kumtumia mtu.

Alimaliza kwa kusema hivyo mkali huyo alipokuwa anafaniwa mahojiano katika kipindi flani cha televishen usiku wa kuamkia leo.

Unaweza kuisikiliza ngoma hiyo mpya ya mkali huyo.

BILLNASS FT YOUNG KILLER & STAMINA - AJE MWENYEWE

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.