Billnass: Nilimchagua Maua Sama kwenye 'Mazowea' lakini Mwana Fa akiingilia kati. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Billnass: Nilimchagua Maua Sama kwenye 'Mazowea' lakini Mwana Fa akiingilia kati.

Msanii anaefanya vizuri kwa sasa hapa bongo kwenye miondoko ya ku-rap,hapa namzungumzia Billnass ametuweka bayana mtu aliyestaili au sautiambayo aliichagua kuwa katika nyimbo yake ya mazowea.

Akizungumza na host wa kipindi cha 'Ngazi kwa Ngaz' mwanadada Salama Jabiri alimueleza kinaga ubaga kilichotokea mpaka Mwana Fa akahusika kwenye ngoma hiyo.

"Maua ni mshkaji wangu lakini ikija kwenye biashara mimi siletagi tena ushkaji, lazima nifuate management yake na nini. Kwahiyo nikamfuata Mwana FA nikamuambia nina demo ya wimbo wangu nataka uisikilize, sababu mara nyingi pia nyimbo zangu zote Mwana FA huwa nampa anasikiliza sababu naliamini pia sikio lake" Pia Billnass akaendelea kusema.

Nilipompa Mwana FA akasema ‘Maua utampata lakini unaweza kuniachia CD ya huu wimbo ?’ Nikamwachia CD, long time. Wakati anaendelea kusikiliza akapata naona idea, akafanya, yeye sema alifanya mwaka jana. Nilikuwa surprised kwa jinsi ilivyofanyika na mtu kama FA kuweza kufanya verse kwa mapenzi bila mimi kumuomba labda, au mimi kumsumbua alijitolea, hapo tu mimi nikaaminia huu wimbo ni mzuri, unaweza kufanya kitu, na nilivyosikia ile verse ya Mwana FA ikabilisha wimbo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.