Belle 9 aukingia kifua wimbo wake mpya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Belle 9 aukingia kifua wimbo wake mpya

Belle 9 ameukingia kifua wimbo wake mpya ‘Mzuri’ ambao unadaiwa kutofanya vizuri.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakidai wimbo huo haujafanya vizuri tofauti na nyimbo nyingine ambazo msanii huyo amewahi kuziachia.

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Flavour Express cha Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez, Belle amesema wimbo huo umefika pale walipokuwa wanapataka kwa kuwa aliuweka kwenye mtandao wake wa Soundcloud kwa mara ya kwanza ili mashabiki wake wafurahie muziki mzuri lakini amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwenye vitu mbalimbali vya redio wakimtaka awatumie wimbo huo ili waucheze.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa tayari ameshafanya kolabo na Saida Karoli wanasubiri muda muafaka ufike ili waweze kuuachia.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.