Baraka The Prince: Mashabiki msinipangie - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baraka The Prince: Mashabiki msinipangie

Mwanamuziki wa RnB anayetamba na ngoma ya 'Acha Niende' Baraka The Prince amewaonya mashabiki wasimpangie maisha binafsi na kwamba wao kinachowahusu kutoka kwake ni muziki mzuri, video pamoja na kuwaandalia Show za kuwapa burudani.

Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio Barakah ametoa kauli hiyo baada ya siku kadhaa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa msanii anayetafsiriwa kuwa ni hasimu wa msanii mwenzake kutoka katika lebo yao ya Rock Star 4000.

"Wewe kama ni shabiki wangu wa muziki haimaanishi pia ni shabiki wa maisha yangu binafsi, maisha yangu binafsi mniachie. Shabiki wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha? kama mtu niliyepiga naye picha ni binadamu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea". Amesema Barakah The Prince.

Katika hatua nyingine Baraka ameweka wazi kuwa tangu kusajiliwa katika lebo ya Rock Star chini ya Bi. Seven Mosha kumemuongezea nafasi na wigo mpana wa kujulikana ndani na nje ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani kubwa katika maisha yake.

Kwa upande mwingine Barakah amekanusha tetesi za yeye kutengwa katika lebo hiyo.
"Unajua kwenye kampuni kila mtu ana makubaliano yake na mikataba yake, Lady Jaydee ana mkataba tofauti na mimi na pia kazi zinaenda kwa muda. Huu ulikuwa muda wake wa kuachia albamu lakini mimi nilikuwa na 'promote kazi yangu mpya hivyo watu wasiseme kama Rock Star inanitenga kwani hawajui mkataba wangu uko vipi. Wao wakae tuu na kusubiri kazi nyingi" Alisema Barakah The Prince.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.