Banda apeta Kamati ya nidhamu, Ruksa kucheza - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Banda apeta Kamati ya nidhamu, Ruksa kucheza

KAMATI  ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia mechi mbili beki wa Simba, Abdi Banda kwa kosa la kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Aprili 2, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Hiyo inafuatia kikao chake cha leo mjini Dar es Salaam, ambacho mchezaji huyo wa timu ya taifa pia, Taifa Stars alihudhuria na kuhojiwa.

Banda alikuwa mwenye bahati kwa kutotolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumtwanga ngumi Kavilla Jumapili katika mchezo ambao Simba ililala 2-1, lakini mara moja Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kuipa Simba SC ikamzuia kucheza na kulipeleka suala lake Kamati ya Nidhamu.

Hatua hiyo inamaanisha Banda sasa yuko kuendelea kuichezea Simba, kwani tayari amekwishakosa mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC timu yake ikishinda 3-2 na dhidi ya Toto Africans wakioa sare ya 0-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kama pia ilibaini Banda ambaye hakupewa adhabu yoyote na refa kwa sababu hakuona tukio hilo, alifanya kitendo cha aina hiyo kwenye mechi namba 169 kati ya Simba na Yanga iliyofanyika Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akimpiga kiungo Said Juma ‘Makapu’.

Awali, Klabu ya Kagera Sugar iliwasilisha malalamiko dhidi ya kitendo cha beki wa Simba, Abdi Banda kumpiga ngumi kiungo wao George Kavilla wakati akiwa hana mpira, na Mwamuzi wa mechi hiyo kutochukua hatua yoyote.

Kwa vile kosa hilo ni la kinidhamu, Kamati ilimsimamisha Abdi Banda kwa mujibu wa Kanuni ya 9 (5) wakati akisubiri suala lake kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Kamati ya Nidhamu inatarajiwa kukaa wakati wowote wiki ijayo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.