Baada ya Wema kuwatolea povu waigizaji Sakata la Roma........Ray aibuka amchana - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Wema kuwatolea povu waigizaji Sakata la Roma........Ray aibuka amchana

Baada ya wasanii Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wenzao kuchukuliwa na watu wasiofahamika tangu usiku wa kuamkia juzi  wasanii mbalimbali wamekuwa wakitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kupost juu ya kusikitshwa na kitendo hicho, Wema Sepetu akiwa moja kati yao.

Lakini post ya Wema Sepetu ambayo aliiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram imeonesha kutokumfurahisha muigizaji mwenzake ambaye amepost pia katika ukurasa wake wa instagram na kueleza kutokufurahishwa na namna Wema alivyoandika kuhusu ishu hiyo.

==> Wema Sepetu aliandika hivi;
"This Is Scary… Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla… Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino…. Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni…??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake…. 

"Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa…??? Oh God help Us Please… Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu… Tumejawa sana Unafki…!!! All in All namuonea sana huruma Nancy…. 

"Our prayers are with u mama… Inshallah mumeo atapatikana… Tuzidi kumuomba Mungu…..πŸ™πŸΌπŸ™πŸΌπŸ™πŸΌ…. Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani….!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino…?? πŸ™„πŸ™„πŸ™„ SMH.. " 

==>Ray Kigosi  hakuipenda post hii, hivyo akajibu;
NAFIKIRI NI VEMA MTU KUELEZA HISIA ZAKE JAPO SIO BUSARA KWA MWENYE HISIA HIZO KUZIELEZA BILA WEREDI NAWASIHI WASANII WENZANGU KUPOTEA KWA ROMA ISIWE SABUNI YA KUTAKATISHA UCHAFU WA MTU SOTE TUMESIKITISHWA NA JAMBO HILO NA TUMEONYESHA KWA VITENDO. MIMI NIMEPOST INSHU YA ROMA TANGU JANA USIKU WEMA SEPETU WEWE ULIKUWA HUJAPOST CHOCHOTE TUSEME ULIKUWA HUNA UCHUNGU? ALAFU LEO UNAANDIKA KUWA BONGO MOVIE HAWAPO PAMOJA NA TUKIO LA ROMA HUKU NI KUTUGOMBANISHA NA WANANCHI WANAOTUAMINI. SISI BONGO MOVIE MARA NYINGI SANA TUNAKUWA PAMOJA KWENYE MATUKIO YA BONGE FLEVA TOFAUTI NA WAO. KAMA UNA UGONVI NA MTU HAYO NI MAMBO YAKO BINAFSI ILA USITUFANYE SISI TUONEKANA WABAYA MBELE YA JAMII UTAKUWA KICHAA KAMA USIPOPATA MAUMIVU KWA TUKIO LA ROMA NIMESIKITISHWA SANA POST YAKO @wemasepetu KAMA UNADHANI HUU NI MUDA MUAFAKA WA KUTAFUTIA POINT KATIKA TUKIO LA ROMA MKATOLIKI UMEFELI HILI NI JANGA LETU SOTE. @wemasepetu #(KINA ROMA WAKO WAPI?).

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.