Arsenal yamfanyia vipimo Kolasinac - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Arsenal yamfanyia vipimo Kolasinac

\
London, England. LICHA ya kocha wa Arsenal, Arsene juzi kukanusha kwamba bado hajamchukua mlinzi wa kushoto wa Schalke, Saed Kolasinac, 23 imedaiwa kuwa staa huyo wa kimataifa wa Bosnia alipimwa afya Arsenal wiki mbili zilizopita.

Kolasinac anamaliza mkataba wake na Schalke Juni 30, mwaka huu na inadaiwa Arsenal imeshinda mbio za kumchukua mbele ya klabu kadhaa zilizokuwa zinamuwana ikiwemo Chelsea ambayo ilikaribia kumchukua dirisha la Januari.

Licha ya hatima ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuwa hewani tayari Arsenal imeanza mikakati ya kumarisha kikosi chao msimu ujao na Kolasinac, ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani atakuwa staa wa kwanza katika kikosi hicho msimu ujao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.