Alikiba Kuuzimikia Wimbo wa 'Kwetu, Raymond Afunguka Haya ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba Kuuzimikia Wimbo wa 'Kwetu, Raymond Afunguka Haya !

Alikiba alijikusanyia pointi tatu mapema wiki hii kutoka upande wa hasimu wake Diamond baada ya kuonekana akiimba wimbo wa Raymond ‘Kwetu’.

Akiongea na kipindi cha Dj Show cha Radio One, kitendo hicho kimeonyesha kumfurahisha kinda huyo kutoka lebo ya WCB ambao ni mahasimu wakuwa wa hitmaker wa Aje.

“Nimefurahi sana kwa sababu wale ndio watu walioanza muziki kitambo na ukiona wanapenda unachokifanya inaonyesha njia nzuri uendelee kukaza ili uendelee kuwagusa mashabiki wengi. Inanipa moyo niendelee kukaza zaidi na zaidi,” amesema Rayvanny.

Hii ni hatua nzuri kwa Ray kwani alishawahi kusema hakuna tatizo hata akifanya wimbo na Alikiba japo hawapikiki chungu kimoja na bosi wake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.