Yanga yashindwa kufika kileleni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Yanga yashindwa kufika kileleni

YANGA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Sare hiyo inayokuja siku moja baada ya mahasimu wao, Simba kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu jana inawanyima nafasi nzuri ya kupanda kileleni Yanga.

Yanga inafikisha pointi 53 baada ya kucheza mechi 24 ikiendelea kuzidiwa pointi mbili na Simba SC yenye pointi 55 za mechi 24 pia. 

Simon Msuva alipoteza nafasi nzuri ya kuifungia Yanga bao la mapema tu dakika ya 35 baada ya kupiga juu shuti la mkwaju wa penalti, kufuatia Ally Lundenga wa Mtibwa Sugar kuunawa mpira kwenye boksi.

Sifa zimuendee mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa aliyempisha kwa mbele Lunenda wakati beki Oscar Joshua anarusha mpira na mchezaji huyo wa Mtibwa akaunawa mpira kwa bahati mbaya.

Pamoja na penalti hiyo, timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu kwenye mchezo huo ambao ulipoozeshwa na hali mbaya ya Uwanja wa Jamhuri licha ya ukarabati uliofanyika.

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Shaaban Nditi, Haroun Chanongo/Kevin Friday dk75, Stahmil Mbonde/Hussein Javu dk83, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Ally Lundenga, Salim Abdallah, Mohammed Issa, Jaffar Ally, Ally Shomary na Ally Makarani. 

Yanga SC; Deogratias Munishi ‘Dida’, Hassan Hamisi, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Kevin Yondan/Said Juma ‘Makapu’ dk70, Simon Msuva, Justine Zulu, Obrey Chirwa, Malimi Busungu/Juma Mahadhi dk31 na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk60.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.