Yanga kwenye mtihani mzito - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Yanga kwenye mtihani mzito

KULEKEA kwenye mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Azam FC, benchi la ufundi la Yanga lipo kwenye mtihani juu ya kupanga kikosi chake kitakachokuwa na uhakika wa kupata ushindi.

Yanga haitakuwa na huduma ya mabeki wake, Kelvin Yondani na Hassan Kessy ambao wote hao wataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Mbali na hao, pia Yanga itamkosa mshambuliaji wake Mrundi, Amis Tambwe ambaye anauguza majeraha.

Kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, aliiambia Nipashe kuwa hiyo ni changamoto kwa benchi lake la ufundi lakini wanapaswa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kesho wanaibuka na ushindi.

"Bado kuna wachezaji wengine ambao wanaweza wakacheza kwenye namba husika, mambo kama haya yanatokea kwenye timu,huwezi ukawa na wachezaji wako wote wakiwa fiti kwenye baadhi ya mechi," alisema Lwandamina.

Lwandamina alisema taarifa nzuri kwao ni kurejea kwa mshambuliaji wao, Donald Ngoma ambaye jana alitarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake.

Nyota huyo juzi alitumia masaa mawili kufanya mazoezi ya peke yake akikimbia kuzunguka uwanja kwa zaidi ya saa moja kabla ya kuanza kufanya mazoezi ya viungo.

Bossou hati hati

Beki huyo aliyekwenda nchini kwakeTogo kuitumikia timu yake ya taifa, alikuwa akitarajiwa kurejea nchini jana kama tu uongozi wa Yanga ungekuwa umemtumia tiketi ya ndege yeye ni mke wake.

Mpaka kufikia juzi jioni Bossou hakuwa ametumiwa tiketi hizo.

Kama Bossou atatua nchini kwa wakati ana nafasi kubwa ya kucheza pamoja na nahodha, Nadir Haroub 'Cannavaro' kwenye safu ya mabeki pamoja na Juma Abdul na Mwinyi Haji.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.