Wizara ya Viwanda yaikana ‘tweet’ ya Mwijage - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wizara ya Viwanda yaikana ‘tweet’ ya Mwijage

Wizara ya Viwanda, Biashara ya Uwekezaji imetoa taarifa kuhusu akaunti ya Twitter inayotumia jina la waziri wa wizara hiyo, Charles Mwijage kuwa sio yake na ujumbe ambao inaandika una lengo la kumchafua waziri huyo pamoja na wizara hiyo kwa ujumla.

Taarifa hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu akaunti hiyo kuweka ujumbe ambao unalaani kitendo alichokifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kwenda Clouds Media akiwa na askari wenye silaha za moto.

Ujumbe huo ulisomeka, “Kilichotokea kwa Clouds Media ni kitendo cha kinyama na wala si uungwana kabisa tunajenga nchi ya viwanda na si ya kutishiana.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.