Wema Ajadiliwa Msikitini - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Ajadiliwa Msikitini

DAR ES SALAAM: Makubwa! Wema Isaac Sepetu amezua gumzo baada ya kujadiliwa kwenye msikiti mmoja uliopo Mwenge jijini Dar kufuatia mhadhiri mmoja maarufu aliyefahamika kwa jina moja la Mwaipopo kuelezea namna mwanadada huyo alivyotoa mchango wake kumsaidia marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ alipokuwa mgonjwa.

Akizungumza kwenye msikiti huo akiwataka Waislam wamchangie fedha kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, mhadhiri huyo alisema kuwa anawashangaa Waislam kutokuwa na mioyo ya kuwasaidia wenzao wanapokuwa na matatizo wakati dini haitaki hivyo.
“Nimezunguka sana kwenye misikiti mingi lakini msaada ambao nimekuwa nikipata kutoka kwa Waislam wenzagu haukuwa wa kuridhisha, inasikitisha sana.
Kuna wakati yule msanii wa filamu, Sajuki alipokuwa anaumwa, akina Wema walimchangia mapesa na akaenda kutibiwa lakini sisi tumekuwa wagumu katika kutoa,” alisema mhadhiri huyo.
Baada ya kusema, hivyo baadhi ya watu waliokuwa msikitini hapo walianza kunong’ona chinichini wakimjadili Wema huku wengi wakisema kuwa inakuwaje staa huyo awe na moyo wa kutoa kushinda waumini wa Kiislam wengine ambao wamejaliwa utajiri. “Wewe fikiria kama Wema ameweza kutoa pesa zake nyingi tu kusaidia katika matibabu ya Sajuki kipindi kile, Waislam kwa nini tunakuwa wagumu,” alihoji kijana mmoja aliyekuwa msikitini hapo.
Hata hivyo, hoja ya mhadhiri huyo ambaye historia yake inaonesha alikuwa Mkristo ni kwamba, Waislam wanatakiwa kusaidiana katika shida na raha pamoja na kwamba alikosolewa kuwa aliyemsaidia Sajuki fedha nyingi kipindi kile hakuwa Wema bali alikuwa ni Jacqueline Wolper.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.