Watumishi 2,059 Watinga Dodoma Awamu ya Kwanza..!!! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Watumishi 2,059 Watinga Dodoma Awamu ya Kwanza..!!!

Jumla ya watumishi wa umma 2,059 wameripoti Dodoma katika awamu ya kwanza ya kuhamia mjini humo  ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati akikabidhiwa uenyekiti wa CCM, Julai 22, mwaka jana.

Awamu ya kwanza ya Serikali kuhamia makao makuu Dodoma inajumuisha mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao, baadhi ya wakurugenzi pamoja na wasaidizi wachache.

Hayo yamebainishwa jana (Ijumaa) katika kikao cha kazi cha mawaziri na naibu mawaziri kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma chini ya uwenyekiti wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.