Uwoya Amshukuru JK kwa Hili - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Uwoya Amshukuru JK kwa Hili

Muigizaji Irene Uwoya amemshukuru Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuwathamini na kuwaamini wanawake kwa kuwapa nafasi za juu katika kuongoza taifa la Tanzania.

Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa hawezi kumsahau Rais huyo kutokana na uamuzi wake wa kutoa nafasi kubwa kwa wanawake katika serikali yake, zikiwemo nafasi za uwaziri, majaji na hata Spika wa bunge, na kwamba, Rais huyo ndiye aliyempa motisha ya kugombea ubunge.

"Namshukuru sana Rais mstaafu... Mh. JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa kutupa wanawake heshima na kututhamini... Alitupa nafasi nyingi sana katika nafasi za mawaziri, majaji na spika... Na hata mimi kama msanii nilihamasika na kuona naweza kugombea ubunge... Kiukweli amefungua njia na ameweka mwanga mkubwa kwa viongozi wengine na wao wakaendelea kuthamini na kuheshimu mchango wetu katika jamii ndiyo maana hata tukapata makamu wa Rais mwanamke kwa mara ya kwanza Tanzania". Amesema Irene

Katika hatua nyingine, Uwoya ameungana na wanawake wengine duniani kusherehekea siku ya wanawake, huku akionesha kukerwa na wanaume wanaowadharau wanawake huku akiongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika jamii na kwamba mwanamke ni mlezi na pia wakati mwingine husimama kulisha familia.

"Mwanamke ndiye mama wa taifa... Ndiyo maana Marekani mwaka 1911 iliadhimishwa siku ya wanawake duniani ambapo vikundi tofauti vya wanawake viliungana kupinga ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa jinsia hususani sehemu za kazi... " Ujumbe wa Irene Uwoya.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.