Usichokijua Kuhusu Dully Sykes na Baraka Da Prince - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Usichokijua Kuhusu Dully Sykes na Baraka Da Prince

Ni ukweli usiofichika kwamba Baraka Da Prince ni mmoja kati ya wasanii wakali ambao huwezi kuacha kuwataja endapo utataja list ya wasanii A List katika muziki wa Boongo Fleva.
Anamiliki hits kibao pamoja na mengine mengi ambayo ameyafanya na kufanikiwa kuchukua nafasi aliyonayo katika game ya music.

Kama umekuwa ukifuatilia page ya instagram ya legendary wa muziki Tanzania Prince Dully Sykes kwa takriban wiki sasa naamini utakuwa umeona kitendo cha legendary huyo kuweka picha ya msanii Baraka Da Prince kwenye profile picture ya page yake hiyo.

Maswali mengi yalikuja kwenye vichwa vya wadau wengi na kupelekea wengine kufukiria mbali zaidi na kuhisi kuwa huenda kuna collabo ambayo inakuja baina ya wawili hao.

Jana kupitia page hiyo hiyo ya instagram Dully Sykes ametusanua kitu ambacho wengi tulikuwa hatukifahamu kuhusu yeye na Baraka Da Prince.

Dully aliandika hivi kwenye page yake “Kuna siku ila mwaka sikumbuki nilipata simu kutoka kwa kijana aliejitambulisha kwa jina la BARAKA” Akanisalimia na kunambia anahitaji nimpatie jina ili alitumie kwenye sanaa….nikamuuliza anaishi wapi?…akanambia anaishi MWANZA…nikamwambia nitampatia jina moja kati ya majina yangu…..ndipo nikampatia “PRINCE nikamwambia ajiite ….BARAKA DA PRINCE na kweli….nashukuru mungu yamekua na amekua mmoja kati ya wasanii wanaonipenda na kuniheshimu…. @barakahtheprince_ nakupenda sana mdogo wangu!…”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.