UEFA: Manchester City Yakwama Dhidi ya Monaco - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

UEFA: Manchester City Yakwama Dhidi ya Monaco

Pep Guardiola ameyaaga mashindano.

Manchester City imeondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa sheria ya magoli ya ugenini katika mechi ya kukata na shoka dhidi ya Monaco. Mechi hiyo ilimalizika kwa magoli 3-1 lakini kwa jumla ya mabao 6-6.

Monaco na Manchester City walionesha mchezo wa kuvutia na kusisimua, wakianza mchezo wa duru ya pili Man City wakiwa mbele kwa mabao 5-3.

Kipindi cha kwanza, kiliongozwa na Monaco. Fabinho, Tiemue Bakayoko na Bernardo Silva walitawala eneo la kiungo, huku Kylian Mbappe akitishia ngome ya City kila wakati.

Na ni Mbappe ambaye baba yake ana asili ya Cameroon ndio aliandika bao la kwanza katika dakika ya saba baada ya kuunganisha krosi ya Silva.

City hawakuweza kujibu mapigo na katika dakika ya 27, Monaco walijikita mbele kwa kuandika bao la pili.

Goli kwa mara nyingine tena lilitokea upande wa kushoto, Thomas Lemar akilisha mpira mtamu kwenda kwa Benjamin Mendy ambaye alichonga krosi iliyopachikwa kimyani na Fabinho.
Kylian Mbappe alitikisa ngome ya City
Monaco walishindwa kwenye fainali Ligi ya Mabingwa 2004

Baada ya mapumziko City walionekana kubadilika, wakitumia mabeki wao kupanda. Lakini walipoteza nafasi kadhaa, Sergio Aguero akipoteza nafasi nyingi, kabla ya Leroy Sane kufunga goli katika dakika ya 71.
Manchester City walifika nusu fainali msimu uliopita wakiwa na Manuel Pellegrini

Mchezo ulimalizika kwa mabao 3-1.

Atletico yaenda robo fainali

Katika mchezo mwingine Atletico Madrid wameingia robo fainali baada ya mchezo wao dhidi ya Bayer Leverkusen kumalizika kwa sare ya 0-0.

Atletico walimaliza kazi yao katika mchezo wa kwanza kwa kupata ushindi wa mabao 4-2.

Droo ya robo fainali itatangazwa siku ya Ijumaa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.