TP Mazembe Yamtimua Kocha wao - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

TP Mazembe Yamtimua Kocha wao

KLABU ya TP Mazembe ya DRC imeachana na kocha Mfaransa, Thierry Froger baada ya kutolewa katika hatua hatya ya 32 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na CAPS United ya Zimbabwe kwa mabao ya ugenini, ikitoa sare ya 1-1 Lubumbashi na 0-0 Harare.

Mazembe imeangukia katika kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na itamenyana na JS Kabylie ya Algeria baada ya droo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri.

Mechi za kwanza zinatarajiwa kucheza wikiendi ya Aprili 7 hadi 9 na marudiano yanatarajiwa kuwa wikiendi ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu.

Froger alijiunga na Mazembe Februari 15, siku chache kabla ya kumenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mechi ya Super Cup ya CAF, akichukua nafasi ya Mfaransa mwenzake, Hubert Velud aliyeondoka mwishoni mwa mwaka jana kuhamia Etoile du Sahel ya Tunisia.

Wasiwasi juu ya mustakabali wa Froger ulianza mapema tu baada ya kushindwa kuwawezesha mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho kubeba Super Cup ya CAF kufuatia kufungwa 1-0 na Mamelodi Februaeri 18, mwaka huu Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria, Afrika Kusini.

RATIBA KAMILI YA MECHI ZA MCHUJO WA KUWANIA 
KUINGIA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO
Yanga SC (Tanzania) vs MC Alger (Algeria)
TP Mazembe (DRC) vs JS Kabylie (Algeria)
AC Leopards (Kongo) vs Mbabane Swallows (Swaziland)
FUS Rabat (Morocco) vs MAS Fez (Morocco)
Rangers (Nigeria) vs Zesco (Zambia)
Mounana (Gabon) vs ASEC Mimosas (Ivory Coast)
RC Kadiogo (Burkina Faso) vs CS Sfaxien (Tunisia)
Bidvest (Afrika Kusini) vs Smouha (Misri)
CNaPS (Madagascar) vs Recreativo do Libolo (Angola)
KCCA (Uganda) vs El Masry (Misri)
Ports Authority (Gambia) vs Hilal Obeid (Sudan)
Port Louis (Mauritius) vs Club Africain (Tunisia)
Rivers United (Nigeria) vs Rayon Sports (Rwanda)
BYC (Liberia) vs Supersports (Afrika Kusini)
AS Tanda (Ivory Coast) vs Platinum Stars (Afrika Kusini)
Horoya (Guinea) vs Ittihad Tangier (Morocco)

(Mechi za kwanza zinatarajiwa kucheza wikiendi ya Aprili 7 hadi 9 na marudiano yanatarajiwa kuwa wikiendi ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu)

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.