Sakata la Askofu Gwajima na Polisi Lachukua Sura Mpya, Hiki Ndicho Kimetokea...!!! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sakata la Askofu Gwajima na Polisi Lachukua Sura Mpya, Hiki Ndicho Kimetokea...!!!

Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.

Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na kupekuwa na kupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo.

“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,”amesema Kibatala.

Aidha Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema “Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo, baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.