Profesa Jay akana kumchana Afande Sele kwenye Kibabe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Profesa Jay akana kumchana Afande Sele kwenye Kibabe

Rapper Profesa Jay amekana kumchana Afande Sele kwenye wimbo wake mpya wa Kibabe.
Jay anatuhumiwa kuandika mstari ambao unaonekana kumgusa Afande kwenye wimbo huo. “Usipo nisikia leo ujue kesho narudi, mwambieni mfalme wenu siti yangu aifute vumbi,” amerap Profesa kwenye wimbo huo.
Akiongea na E News ya EATV, rapper huyo amekana kwa kusema, “Afande Sele mimi ninamheshimu toka yupo Chadema kabla hajaenda ACT na hata wakati tunaanza harakati za kugombea kila mmoja alimtakia mwenzake kila la kheri.”
“Kingine mimi mpaka leo mtu nayemheshimu katika utunzi wa mashairi nikiwataja kina Jay Moe basi Afande siwezi kumuacha. Alikiba mimi ni mdogo wangu na mimi ni shabiki wake analijua hilo sasa sielewi haya maneno yametoka wapi,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.