Paul Pogba Anusurika Kichapo, Kisa Hiki Hapa ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Paul Pogba Anusurika Kichapo, Kisa Hiki Hapa !

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester United amenusulika kichapo kutoka kwa mashabiki wake baada ya kukataa kusaini Autography.

Kwa mujibu wa vyanzo vingi vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa Pogba akiwa kwenye matembezi jijini Manchester aliingia kwenye mgahawa mmoja uliopo nje kidogo ya jiji na kukutana na mashabiki wake waliompokea kwa Furaha kama ilivyo kwa mashabiki wa soka Duniani.

Ishu ikaja pale ambapo mashabiki hao walitaka wasainiwe vitabu vyao vya kumbukumbu (Autograhy) kitu ambacho Pogba alipokataa na kusababisha tafrani kwa mashabiki hao walioanza kumkwida kiasi kwamba mpaka polisi wakaingilia kati kutuliza ghasia.

Baada ya kashi kashi hiyo Pogba alilazimika kuondoka Mgahawani hapo kwa sababu za kiusalama zaidi lakini hakuna hata mmoja wa mashabiki aliyeripotiwa kukamatwa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.