Nuh Mziwanda: Msinipangie maisha binafsi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nuh Mziwanda: Msinipangie maisha binafsi

Msanii wa wa bongo fleva anayetamba na ngoma ya anameremeta, Nuh Mziwanda amewataka mashabiki zake kutompangia jina la mtoto wake na kusisitiza yeye kama baba ndiye mwenye mamlaka hayo.

Kupitia eNewz ya EATV,  Nuh amefunguka kwamba hawezi kumuita binti yake majina ya kizungu kwa madai kuwa siku akikua na kwenda kwenye asili yake atakutana na hayo majina hivyo hakuna haja ya kumpatia mtoto majina yasiyo ya asili kwani hata mastaa wakubwa wana majina ya asili lakini wanaingiza pesa akimtolea mfano Iyanya na wengineo

"Mimi ndiyo baba wa mtoto ninatakiwa kujua jina la mtoto, nimempatia binti yangu jina la mama yangu mzazi ambaye kwa kifupi namuita Anya, hii ni damu yangu mimi kwa atakayeona jina halimpendezi ni yeye tu lakini mimi najivunia na ninalipenda" - alisema Nuh

Katika hatua nyingine Nuh amesema kuwa japo kuwa wakwe zake hawakupendezwa na yeye kushirikiana na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Shilole katika kazi iliyowafanya wazunguke mikoa tofauti tofauti lakini wanapaswa kuelewa yeye kama mzazi mwenye familia lazima apambane kuhakikisha familia yake inaishi maisha mazuri.

"Siku naenda kumuoa binti yao walijua kabisa mimi ni msanii lakini suala la mimi kufanya kazi na Shilole wao ni watu wazima wanapaswa kujua kwamba mimi natafuta pesa ili  mtoto wao ale na mwanangu pia sitaki familia yangu iishi mazingira mabovu ndiyo maana napambana na maisha yawe mazuri" - Nuh aliongeza

Aidha Nuh ameongeza kuwa pamoja na maneno yanayozagaa yeye na wakwe zake wana mahusiano mazuri.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.