Nisingekubali Mwana Fa Aimbe Kama Angenambia Mapema - Mzee Mwinjuma - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nisingekubali Mwana Fa Aimbe Kama Angenambia Mapema - Mzee Mwinjuma

Mwana Fa ni moja kati ya majina makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya upande wa hiphop ambao wanasifiwa kwa uandishi mzuri wa mistari yake,Mwana Fa pia ni mmoja kati ya watu wenye tungo ambazo baadae huleta maneno mtaani.

XXL ya Clouds FM imempata baba mzazi wa Mwana Fa anayeitwa Mzee Mwinjuma ambaye naye ni muimbaji wa muziki wa bendi alipoulizwa kama Mwana Fa kama aliwahi kumshirikisha wakati anaanza muziki wake amesema kuwa hakumwambia na kama angemwambia asingemkubalia kwa kipindi hicho cha nyuma.

Mzee Mwinjuma amesema>> ’Mimi nisingekubali ana bahati nilikua nje ya nchi,unaona maisha ya muziki wetu vile tulivyokuwa tunapiga ilikua ni taabu sana,kulikua hakuna pesa wao kwa sasa ni kama tumewafagilia njia tu’

‘Sidhani kama ningeng’ang’ania yeye afanye muziki kwa sababu sikua najua mabadiliko gani yanakuja huko mbele ya safari’
– Mzee Mwinjuma.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.