Nick wa Pili awachana wasanii wenzake, awapa tano vyombo vya habari - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nick wa Pili awachana wasanii wenzake, awapa tano vyombo vya habari

Rapper Nick wa Pili amefurahishwa na umoja uliooneshwa na vyombo vya habari katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na hali tete baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia kituo hicho Usiku wa Ijumaa iliyopita kutokana na video za CCTV kamera zilivyoonyesha.

Nick ametoa pongezi hizo kupitia mtandoa wa Twitter lakini pia amewachana wasanii wenzake ambao wamekuwa hawana umoja katika kutafuta maslahi yao.

Kupitia mtandao huo, rapper huyo ameandika:

Hongera vyombo vya habari kuungana, wasanii sisi mwenzetu hata auwawe, tutatizama tu..kimtizamo finyu…

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.