Nay wa Mitego aongea kitu kuhuhu Vanessa Mdee na sakata la dawa za kulevya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay wa Mitego aongea kitu kuhuhu Vanessa Mdee na sakata la dawa za kulevya

Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego amefunguka kwa kumpa pole mwanadada Vanessa Mdee ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kutumia na kusambaza dawa za kulivya.
Muimbaji huyo alijisalimisha kwa jeshi la polisi siku 5 zilizopita baada ya kutajwa kwenye list ya RC Makonda ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kujisalimisha polisi central kwajili ya mahojiano.
Rapper huyo ameonyesha kuguswa na tukio hilo lililomtokea muimbaji huyo wa wimbo Cash Madame huku akimtaka kuvumilia kwa yote yanayoendelea.
“Vanessamdee Sijui ulipo anzia, but mpaka apa ulipofikia umepambana sana. Nina imani mungu ndo aliye kufanyia wepesi mpaka kua #BrandKubwa na kupata hatua Ulizo nazo. Naamini Mungu Huyu Huyu ndiye atakae kufanyia Wepesi Kwenye yanayo kukabili ivi sasa. Amini izi ni Changa moto tu na ni Mapito ambayo Binadamu tunapitia kwenye Safari ya kuelekea kutimiza Ndoto zetu,” aliandika Nay Instagram.
Aliongeza, “I pray for you my friend Vanessa, naamini brand yako haiwezi haribika kirahisi kwa sababu umepambana sana ni wasichana wachache wenye kuweza ku-fight kama wewe. Mungu ata kusimamia uzidi kusonga mbele, Haya yata pita nina imani utakua strongZaidi. #CashMadame KeepItUp. Napenda kuona Wasichana wakifanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii #VannesaTheBrand wewe ni mwanamke wa shoka. Usiyumbishwe kuwa Mfano. Najivunia uwepo wako kwenye Game,”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.