Nape aikanusha akaunti feki ya twitter - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nape aikanusha akaunti feki ya twitter

Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameukanusha ujumbe unaotumwa kupitia akaunti ‘feki’ ya twitter yenye jina lake na kuwataka wanaofanya hivyo waache kwani anawafahamu na atawataja.

Nape ameandika hayo leo  sita mchana baada ya akaunti hiyo feki kuandika:

“Amemzuia Kinana kuzungumza, akae akijua hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”

Akaunti hiyo feki  pia iliandika:

“Siyo wote wenye nidhamu ya woga kunyamazia udhalimu unaowafanyia, utawazuia watu kuzungumza hadi lini? Katibu wangu piga moyo konde”

 Nape alikanusha na kuandika:

“Mnahangaika nini kunichafua kwenye twitter, hizi tweet zinazosambwa za maneno yasiyo na busara siyo zangu, nilishasema jana nikamaliza, nitawataja sasa!”

 Leo asubuhi Nape aliandika ujumbe wa kuwashukuru wanahabari na kusema alikuwa hajui kama wanampenda kiasi kile.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.