Mwanamitindo wa Marekani afariki dunia kwa kugongwa na treni wakati wa photoshoot - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwanamitindo wa Marekani afariki dunia kwa kugongwa na treni wakati wa photoshoot

Mrembo wa miaka 19 aliyefahamika kwa jina la Fredzania Thompson amegongwa na treni wakati akipiga picha.
Fredzania alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha Blinn na alikuwa na ndoto za kuwa mwanamitindo mkubwa duniani. Mzazi wa mrembo huyo, Akamie Stevenson ameliambia shirika la habari la CNN, “Bila shaka hilo ndio jamba ambalo alilokuwa akilitaka kulifanya katika maisha yake. Ndiyo shughuli aliyoanza kuifanya siku aliyofariki dunia.”
Hata hivyo msemaji wa polisi wa Navasota, Justin Leeth amesema mpaka sasa hawajagundua tatizo lolote juu ya kifo hicho kama kilikuwa cha hila yoyote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.