Msanii Hussein Machozi Aeleza Sababu za Kuficha Mahusiano Yake ya Kimapenzi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Msanii Hussein Machozi Aeleza Sababu za Kuficha Mahusiano Yake ya Kimapenzi.

Hussein Machozi ni msiri mkubwa kwa sasa katika ile sekta mashuhuri ya malavidavi.

Mkali huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akiishi nchini Italia amesema sababu kubwa ya kutoyaweka sana mahusiano yake hadharani ni kutokana na kuamua kuyaweka pembeni na kazi zake.

“Kiukweli ni kwamba yupo, lakini huwa sipendi kuweka mahusiano yangu hadharani. Muziki wangu hauhusiani kabisa na mahusiano yangu. Hayo ni maisha yangu kabisa binafsi,” Machozi alimjibu shabiki kwenye video aliyoiweka Instagram.

“Hata mwenyewe ambaye niko naye huwa hapendi hata kutokea kwenye gazeti, hanaga social network,” aliongeza.

Muimbaji huyo hivi karibuni amepanga kuachia wimbo wake mpya baada ya kuwa kimya kwa muda.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.