Mourinho: Pogba Anaonewa 'Wivu' na Wakosoaji - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mourinho: Pogba Anaonewa 'Wivu' na Wakosoaji

Meneja Jose Mourinho na Paul Pogba

Kukosolewa kwa Paul Pogba kwa hivi majuzi ,kumechochewa na 'wivu' na wanaomlenga kiungo huyo wa kati kwa sababu wanahitaji fedha zozote ili wakidhi maisha yao,'' amesema meneja wa Manchester United Jose Mourinho.

Pogba , 24, alitia saini mkataba mwengine na United na kuvunja rekodi ya dunia kwa kitita cha pauni milioni 89 kutoka Juventus mwezi Agosti.

Kiwango cha mchezo cha kiungo huyo wa kati wakati mwengine kimekuwa cha chini msimu huu.

''Si makosa ya Pogba, wakosaji wengine wako taabani, huko Paul akiwa milionea,'' amesema Mourinho.

Nahisi kwamba ulimwengu unapoteza thamani yake ,nahofia kiwango cha wivu unaoingia. Si makosa ya Paul kwamba anapokea pesa mara kumi zaidi ya wachezaji wengine waliokuwa hapo awali. Ameongezea Mourinho.

''Paul alifika kileleni na hakuna mtu alimpatia chochote . Nina wasiwasi jinsi mambo yanavyoendelea na hata kwa vizazi vijazo. Wivu uko kila mahali.''

Pogba ambaye amefunga magoli saba na kutoa usaidizi mara tano katika mechi 40 msimu huu, alipokonywa umaarufu huo na N'Golo Kante , baada ya kushindwa na Chelsea katika kombe la FA hatua ya robo fainali.

Baada ya mchuano huo , kiungo wa kati wa Chelsea Frank Lampard , alisema Kante ni kiungo wa kati bora duniani, na meneja wa zamani wa Uingereza na mchambuzi wa BBC Alan Shearer amesema: ''Nadhani mnatafuta mwaandishi wa soka wa mwaka na mchezaji bora wa mwaka''

Akizungumza kabla ya mchezo wa United dhidi ya Rostov katika ligi ya Uropa hatua ya timu kumi na sita bora siku ya Alhamisi , walipotoka sare ya 1-1 ,Mourinho alisema ''anafuraha sana'' na matokea ya Pogba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.