Mniache na Nuh Mziwanda -Shilole - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mniache na Nuh Mziwanda -Shilole

Hayo yamekuja baada ya kuzagaa kwa picha zinazowaonesha wakiwa pamoja katika mapozi ya kimapenzi jambo ambalo Shishi amesema siyo la kweli ila watu ndiyo wanavumisha hivyo vitu.

"Mimi na Nuh ni washikaji tu, halafu Mwanza hatujakatana katika 'show' ila kila mtu alikuwa kwenye mishe zake hivyo sijaona tatizo la mimi kusalimiana naye pamoja na kupiga picha kwa kuwa alikuwa 'Ex boyfriend' wangu na nimeishia naye takribani miaka 5 watu waache tabia ya kukuza vitu ambavyo hawana uhakika navyo". Alisema Shilole kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EA Radio

Aidha Shilole amesema anampenda Barnaba kwa kuwa ndiyo mtu pekee anayemsaidia katika kuandika mashairi ya wimbo ambazo anazitoa hata 'Hatutoi kiki' ameandika msanii huyo.

Kwa upande mwingine Shishi baby amewataja wasanii wake watano anaowakubali kila wakati kusikiliza ngoma zao wakiongozwa na malkia wa taarabu Khadija Kopa, Mwasiti, Linah, Diamond Platnumz pamoja na Rayvanny.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.