Mikopo ya Coca Cola Yagunduliwa Kuwa na Kinyesi cha Binadamu.
Polisi wameanzisha uchunguzi wa kile kilichoonekana kuwa kinyesi cha binadamnu, kupatikana kwenye mikebe ya kujazwa soda iliyowasilishwa kwa kiwanda cha Coca Cola huko Ireland kaskazini.
Shughuli za usiku katika kiwanda cha Lisburn zilivurugwa wiki iliyopita wakati mashinde zilikwama.
Kampuni hiyo ilisema kuwa kisa hicho hakikuathiri vinywaji vyovyote ambavyo kwa sasa viko sokoni.
Polisi wanachunguza ripoti kuwa mikebe mingi huenda ilichafuka.
Coca-Cola ina kiwanda kikubwa huko Lisburn
Kiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, Lisburn
Msemaji wa Coca-Cola amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifahamu kisa hicho cha mikebe mitupu katika kiwanda cha Knockmore.
"Tatizo hilo lilitambuliwa mara moja na bidhaa zote zilizoathirika kuzuiwa na haziwezi kuuzwa. Hiki ni kisa kilicho kando na hakiathiri biddaa zozote zilizo sokoni" msemaji wa Coca Coa alisema.
Download App Yetu MPYA >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !
No comments
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.