Mashabiki wa Muziki Wamdhihaki Diamond Mtandaoni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mashabiki wa Muziki Wamdhihaki Diamond Mtandaoni

MASHABIKI  wa muziki wa  Bongo Fleva nchini wamekuwa wakisambaza picha ya mwanamuziki nyota, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’,  ikimuonyesha akiwa katika hali duni tofauti na ukwasi alionao hivi sasa.

Mashabiki hao wamekuwa wakiisambaza picha hiyo kwa lengo la kumdhihaki ili kuonyesha kuwa maisha huanzia mbali,  hivyo watu wasisahau walikotokea.

Picha hiyo imekuwa ikisambazwa pamoja na ujumbe tofauti hivyo kuwaudhi  mashabiki wa mwanamuziki huyo na kuwafurahisha mahasimu wake.

Aidha  picha hiyo inawaonyesha Diamond na mwigizaji Irene Uwoya ambapo Diamond anaonekana katika taswira ya kijana mwenye hali duni tofauti na alivyo hivi sasa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.