Manchester United Kumkosa Rooney Dhidi ya Chelsea. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Manchester United Kumkosa Rooney Dhidi ya Chelsea.

Manchester United hawatakuwa na mshambuliaji namba moja dhidi ya Chelsea.

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney ameondolewa katika kikosi kitakachomenyana na Chelsea katika hatua ya robo fainali kombe la FA itakayopigwa leo hii.

Rooney aligongana na mlinzi Phil Jones wakati wa mazoezi na kupata majeraha katika mguu wake, huku Zlatan Ibrahimovic akianza kutumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings.

Washambuliaji Anthony Martial na Marcus Rashford nao pia watakosa mchezo huo kwa kuwa ni wagonjwa.
Zlatan Ibrahimovic (kulia) nae pia atakosa mchezo huo.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema wachezaji wa kikosi chake wote ni wazima.

Manchester united hawatakuwa na mshambuliaji wa kikosi cha kwanza leo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.