Man city yapigwa faini ya pauni elfu 35 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man city yapigwa faini ya pauni elfu 35

Ilikuwa ni miongoni mwa michezo ya kusisimua zaidi EPL

Klabu ya Manchester City imetozwa faini ya paundi alfu 35 kufuatia kulalama mbele ya mwamuzi wakati alipotoa adhabu ya penalti kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Klabu ya Man city imepewa onyo kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wake kuwa na nidhamu uwanjani kiasi cha kumzonga mwamuzi kila wakati.

Hii inafuata tukio la dakika ya 50 baada ya mwamuzi Michael Oliver kuizawadia Liverpool mkwaju wa penalti.

James Milner aliandika bao kwa mkwaju huo wa penalti huku Sergio Aguero akisawazisha dakika ya 69.

Katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 Gael Clichy alimchezea vibaya mshambuliaji Roberto Firmino wa liverpool na kusababisha penalti hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.