Malaika apewa jina jipya na Wamarekani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Malaika apewa jina jipya na Wamarekani

MKALI wa Ngoma ya Rarua, Diana Exavery ‘Malaika’ ameamua kulikubali rasmi jina la Sinyora baada ya raia wa Tanzania waishio Marekani pamoja na baadhi ya Wamarekani kumbadilisha jina.

Akizungumza kwa njia ya WhatsApp moja kwa moja kutoka Washington DC, Sinyora alisema kwa sasa hatalitumia jina la Malaika tena na badala yake ataheshimu mawazo ya watu hao waishio Marekani.

“Kukaa kwa miezi kadhaa hapa Marekani ni heshima tosha, wananikubali na nimelikubali moja kwa moja jina la Sinyora kuanzia sasa na siyo tena Malaika,” alisema Sinyora.

Kwa zaidi ya miezi mitatu, Sinyora yupo nchini Marekani kwa ziara ya muziki ambapo hadi sasa ameshafanya shoo sehemu kibao kama vile, Texas, Las Vegas na Washington DC.
Wamarekani.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.