Lissu aachiwa kwa dhamana ya bondi ya Sh10m - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lissu aachiwa kwa dhamana ya bondi ya Sh10m

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo (Ijumaa) imemuachia, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema)  kwa dhamana ya bondi ya Sh10 milioni.

Lissu amedhaminiwa na maelezo ya awali yatasomwa Aprili3, mwaka huu.

Leo asubuhi, Lissu alisomewa mashtaka matano na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi  likiwamo ya kutoa maneno  yenye nia ya kuhimiza hisia za kidini ambayo yangeweza kupelekea uhasama baina ya jamii za Watanzania.

Lissu  ambaye anajiwakilisha yeye mwenyewe mahakamani hapo aliomba maelezo hayo ya awali yasomwe Jumatatu, ili aweze kuhudhuria uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) unaotarajia kufanyika kesho.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.