Linex: Kiki Zinaua Muziki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Linex: Kiki Zinaua Muziki

MSANII wa Bongo Fleva anayetikisa kwa sasa na wimbo wake Kiherehere, Sunday Mangu,‘Linex’, amefunguka kupitia akaunti na kudai kuwa muziki mzuri unapotea ama unakufa kwa uwepo wa kiki (Skendo).
Akipiga stori na mwandishi wa mtandao huu, maskani kwake Mbezi Beach Dar es Salaam Linex amesema kuwa imekuwa kama utamaduni kwa sasa ka wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Muvi pale wanapohitaji kutoa kazi zao za sanaa wamekuwa wakiibuka na skendo mbalimbali wakiamini kazi zao zitapolewa kwa urahisi kwa njia hiyo.
“Nachoweza kusema turudi kushabikia muziki mzuri, tuache kushabikia skendo. Nachokiona hapa muziki unapotea kabisa”alisema Linex
Aidha Linex amewataka mashabiki kurudi katika ushabiki wa muziki mzuri sio kushabikia skendo za watu maarufu. Kitendo cha kushabiki skendo kinaua muziki, pia Linex amewataka wasanii kutofautisha kati ya kazi zao na maisha yao halisi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.