Kutana na Kipaji Cha Pekee Tanzania Mchoraji Emmanuel Mushi ( @ema_truth ) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kutana na Kipaji Cha Pekee Tanzania Mchoraji Emmanuel Mushi ( @ema_truth )

Emmanuel Mushi @ema_truth
Emmanuel Truth akimkabidhi Mh. Said Meck Sadick picha aliyomchora.
Emmanuel Mushi ndilo jina nililopewa na wazazi wangu mnamo mwaka 1993 niliozaliwa. lakini mama yangu mzazi alipenda sana kuniita 'TRUTH' nikiwa teenager nikaamua kulitumia kama jina langu la sanaa. 

Nimepewa karama ya Kuchora na Mungu huyu hakukosea kwani nikitu ambacho nakipenda sana na ninajivunia .Lakini katika yote namshukuru Mungu kwani kanipa na watu ambao wananisimamia na kujitolea kwa hali na Mali ili kusimamia hii Karama nilioyopewa na Mungu, nao ni Mama yangu, pamoja marafiki zangu wa karibu. 
Emmanuel Mushi @ema_truth
Picha ya Hayati Mwl. J.K Nyerere
Kuipenda karama hii nakuijali kunanipa ujasiri wa kuchora vitu mbalimbali na watu mbalimbali mashuhuri Wa Taifa langu hili la Tanzania. Nimewachora watu mbalimbali Mashuhuri ambao pia wamenipa nguvu ya kusonga mbele kuhakikisha nafika levo ambayo naweza kutajwa katikati ya wachoraji Wa Kimataifa. 
Emmanuel Mushi @ema_truth
Baadhi ya kazi za Emmanuel Truth

Lakini zaidi Sana kinachonipa ujasiri wakuwachora mpaka viongozi mbalimbali Wa Taifa langu nikutokana na michango yao katika nchi hii ya Tanzania yaani niwakuigwa.

Picha ya mwisho ya kiongozi kuchorwa ni ya Mkuu wangu Wa mkoa Wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Meck Sadick nikiongozi ambe mkoa wa Kilimanjaro unajivunia kua nae, kutokana na kazi anayoifanya yakuhakikisha mkoa wa Kilimanjaro unakua ni mkoa Wa mfano katika nyanja mbalimbali mfano mzuri katika maswala ya Usafi, Elimu, na Kilimo.
Emmanuel Mushi @ema_truth
Comment ya Jaqueline Mengi 'Klyn' mke wa Reginald Mengi kwenye moja ya kazi ya Ema_Truth
Ni matumaini yangu kwamba kwa uweza wa Mungu nitafika mbali Sana. Na nitakua mtu ambae ni chachu kwa vijana wengine wenye karama kama yangu kutokata tamaa bali kuumba ujasiri nakujiamini ili nao wafikie ndoto zao.

Je Ungependa kuchorwa ama kuchorewa picha ya kitu unachokipenda ? 

Wasiliana na Emmanuel kwa kufollow Instagram @ema_truth 

Simu: +255 652266539

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.