Kinadada wa Arsenal Watupwa Nje Kombe la FA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kinadada wa Arsenal Watupwa Nje Kombe la FA

Marisa Ewers alijiunga na Birmingham City kutoka Bayer Leverkusen Aprili 2016

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA la Wanawake nchini Uingereza, Kinadada wa Arsenal, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu.

Hii ni baada ya kuchapwa 1-0 na kinadada wa Birmingham City katika hatua ya robofainali.

Bao la Birmingham lilifungwa na Marisa Ewers dakika ya 77.

Kipa wa Birmingham Ann-Katrin Berger alifanya kazi ya ziada kuwazuia Arsenal kufunga. Aliokoa makombora kutoka kwa Kim Little, Danielle Carter na Danielle van de Donk kipindi cha kwanza.

Katie McCabe na Jordan Nobbs walishambulia lakini wakashindwa kulenga vyema wavu upande wa Arsenal muda mfupi kabla ya Ewers kufunga.

Droo ya nusufainali itafanyika baadaye Jumatatu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.