Kina Dada wa Arsenal Walaza Tottenham 10 - 0 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kina Dada wa Arsenal Walaza Tottenham 10 - 0

Danielle van de Donk alifungia Arsenal mabao mechi 20 msimu uliopita

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa Arsenal waliwalaza wapinzani wao Tottenham 10-0 na kufika robo fainali Jumapili.

Danielle van de Donk alifungia wenyeji hao mabao matatu, naye mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth Mead akafunga bao pia mechi yake ya kwanza kuchezea Arsenal.

Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0.

Bristol City walilaza Millwall 5-0.

Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda kwenye mechi hizo za raundi ya tano.

Droo ya robo fainali itafanyika baadaye Jumatatu.

Matokeo kamili mechi za raundi ya tano

Manchester City 1-0 Reading (Jumamosi)

Arsenal 10-0 Tottenham

Birmingham 2-0 West Brom

Bristol City 5-0 Millwall

Chelsea 7-0 Doncaster

Liverpool 2-1 (AET) Everton

Notts County 3-2 Yeovil

Sunderland 3-2 Aston Villa

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.